CHAKULA CHA MOTO NI NINI?

 1.4 CHAKULA CHA MOTO (FUEL) 

Ni kitu chochote kinachoweza kuwaka,Vitu hivi vinapatikana katika hali tatu. 

Hali ya ugumu (solids) kama vile karatasi, nguo, majani na plastiki n.k 

Hali ya vimiminika vinavyowaka (flammable liquids) kama vile Spritis, kerosine, 

Grease, Diesel, Alcohols. 

Hali ya Gesi (Gases) kama vile Hydrogen, Butane, Propane, Acetlyene,Coalgas n.k. 

1.5 UKUAJI NA USAMBAAJI WA MOTO

Kuna njia tatu ambazo moto unaweza kusambaa. 

(a) Msafara (Convection) 

Hewa inapopata joto hutanuka na kuwa nyepesi zaidi ya hewa inayotuzunguka na 

huchanganyika na gesi inayotoka kwenye moto na hupanda kwenda juu 

kutengeneza msafara hivyohusaidia moto kusambaa toka sehemu za chini ya jengo 

hadi juu. 

(b) Mnunurisho (Radition) 

Katika njia hii joto husafiri kwakupitia maeneo wazi kama vile mionzi ya jua 

inavyosafiri na kutua juu ya uso wa dunia. Moto pia huweza kusambaa kwa njia hii 

kutokana na joto kusafiri toka kwenye kitu kilicho karibu na moto. 

(a) Mpitisho (Conduction) 

Katika njia hii joto husafiri kwa kupitia kwenye vitu vigumu kama vile chuma. Vyuma 

vilivyotumika katika ujenzi wa paa la jengo huchangia katika kusambaa moto. 

Comments

Popular Posts