FAHAMU MADARAJA YA MOTO
1.7 MADARAJA YA MOTO
Kuna umuhimu mkubwa wa mtu yeyote kufahamu aina ya moto uliotokea ili aweze
kuuzima kwa usalama na usahihi kwa kutumia kizimio sahihi ili kuepuka madhara
yanayoweza kusababishwa na huo moto, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwaka au
kusambaa kwenye sehemu zingine zilizo salama.
Kuna madaraja manne ya moto ambayo ni kama ifuatavyo:
DARAJA LA KWANZA
Hili daraja linahusisha mioto yote yenye asili ya mimea kama vile makaratasi, nguo,
mbao, kuni, majani, miti n.k.
(Hapa kizimio sahihi ni maji)
DARAJA LA PILI
Hili daraja linahusisha mioto ya vimiminika vinavyolipuka na kuwaka kama vile
petroli dizeli mafuta ya taa, rangi ya mafuta, mafuta ghafi, mafuta ya kupikia n.k.
(Kizimio sahihi cha mioto ya vimiminika vinavyowaka ni fomu, unga mkavu, blanketi
ya kuzimia moto, na mchanga mkavu)
DARAJA LA TATU
Daraja hili linahusisha mioto ya gesi kama vile gesi asilia na gesi za viwandani mfano
Songas, Propen, Methen.pia daraja hili utapata mioto inayotokana na kifaa
kinachotumia umeme kuungua.Ikumbukwe kuwa hakuna moto wa umeme ila
umeme ni chanzo kikubwa cha moto.
(Kizimio sahihi ni kufunga valve ya gesi inayotoka kwenye mtungi uliohifadhi gesi.)
Kisha kutumia unga maalumu(DC au DP)
DARAJA LA NNE
DARAJA hili linahusisha mioto inayohusisha vyuma kama vile
Aluminium,Zink,Kopa(copper) ,makaa ya mawe n.k
(Kizimio sahihi ni ‘Unga maalumu.usitumie maji)
Comments
Post a Comment
Karibu Tukuhudumie!