Makala juu ya Elimu ya moto

 1.MOTO(FIRE) 

1.1 Utangulizi 

Kutokana na shughuli mbalimbali za maendeleo ya binadamu, kuna umuhimu wa 

kuwa na elimu juu ya usalama wa moto na namna ya kukabiliana nao mara tu 

unapotokea kwa kuwa moto husababisha upotevu wa maisha,ulemavu na uharibifu 

mkubwa wa mali na hata kusababisha watu kuishi katika hali kubwa ya umaskini. 

1.2 MOTO NI NINI?

Moto ni mgongano/mpambano endelevu wa kikemikali ambao hutoa joto na 

mwanga kutegemea na hali ya mazingira na vitu vinavyoungua au kuwaka. 

1.3 MAHITAJI YA MOTO 

Ili moto uweze kutokea au kuwaka unahitaji vitu vitatu ambavyo ni: 

Hewa ya Oksijeni (OXYGEN) ambayo ni 21% ya hewa yote katika uso wa dunia. 

Chakula cha Moto (FUEL)– hiki ni kitu chochote kinachoweza kuwaka na 

kimegawanyika katika hali kuu tatu zimeainishwa hapo chini.

Joto (HEAT) – ni chanzo cha moto ambapo yaweza kusababishwa na msuguano wa 

vitu mbalimbali / kiberiti ambavyo vyaweza kusababisha moto. 

Hivi vyote vinaitwa pembe tatu za moto. 


Comments

Post a Comment

Karibu Tukuhudumie!

Popular Posts