NJIA ZA KUPAMBANA NA MOTO

 1.6 NJIA AU MBINU ZA KUPAMBANA NA MOTO:

Kuna njia au mbinu tatu za kupambana na moto. 

(a)Kupoza (COOLING). 

Ni kitendo cha kushusha joto la kitu kinachoungua kwa kutumia maji ,Kitendo hicho kitaalamu kinaitwa Cooling .

(b)Kufunika (Smothering).

Maana yake, ni kuzuia hewa ya oksijeni {oxygen} isifike kwenye vitu vinavyoungua. 

Inawezekana kufunika kwa kutumia vitu kama mapovu {foam}, poda kavu {dry powder}, blanketi {fire blanket}, mchanga mkavu ama kitu chochote kinachoweza kufunika moto bila chenyewe kuungua. Kitendo hicho kitaalamu kinaitwa Smothering. 

(c)Kuondoa chakula cha moto, “Fuel” (Starvation).

Maana yake, ni kuondoa vitu vinavyoungua katika vitu visivyoungua au kuondoa vitu visivyoungua katika vitu vinavyoungua. Kitendo hicho kitaalamu kinaitwa Starvation .

Mtu akitumia njia moja wapo kati ya hizo tatu atakuwa amevunja muungano wa pembe tatu za moto na moto utazimika. 

Comments

Popular Posts